TAARIFA
MAADHIMISHO YA MEIMOSI NA JUKWAA LA WALIMU WAZALENDO CHAMWINO
Katika kuazimisha siku ya wafanyakazi Duniani. Jukwaa la Walimu Wazalendo Chamwino, wameungana na wafanyakazi wengine duniani kusherehekea siku hiyo kwa kutembelea kituo cha Afya Chamwino na kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa kituoni hapo.
Aidha kwa kutambua umuhimu wa siku hii Jukwaa limetumia fursa hiyo kuzungumza na watumishi waliokuwa zamu katika kituo hicho, kuwapongeza kwa utendaji mzuri wa kazi na vilevile kuwatia moyo katika majukumu mazito waliyonayo.
Jukwaa linaridhishwa sana na usimamizi mzuri wa sekta mbalimbali zinazotoa huduma kwa wananchi hususani sekta ya Afya. usimamizi huu bora unaofanywa na Serikali ya *Chama Cha Mapinduzi* chini ya Mwenyekiti na Rais Dr. *John Pombe Joseph Magufuli* umeimarisha utoaji wa huduma bora na zenye tija.
Jukwaa la Walimu Wazalendo Chamwino linatia shime kwa Walimu wote Wilayani Chamwino, kuendelea kujituma na kutoa huduma bora zenye tija kwa Umma wa Watanzania
Tunaamini Tanzania yenye Neema itajengwa na Watanzania wenye Uzalendo wanaojitolea na wenye kupambania maendeleo ya Taifa lao.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais wetu *Dr. Magufuli*

Post a Comment